1. Usiku nikiwa kitandani mwangu,niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu;nilimtafuta, lakini sikumpata.
2. Niliamka nikazunguka mjini,barabarani na hata vichochoroni,nikimtafuta yule wangu wa moyo.Nilimtafuta, lakini sikumpata.
3. Walinzi wa mji walinionawalipokuwa wanazunguka mjini.Basi nikawauliza,“Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?”
4. Mara tu nilipoachana nao,nilimwona mpenzi wangu wa moyo;nikamshika wala sikumwachia aondoke,hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu,hadi chumbani kwake yule aliyenizaa.
5. Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,kama walivyo paa au swala,msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,hadi hapo wakati wake utakapofika.