10. Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:Nitaweka sheria zangu akilini mwao,na kuziandika mioyoni mwao.Mimi nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.
11. Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake,wala atakayemwambia ndugu yake:‘Mjue Bwana’.Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
12. Nitawasamehe makosa yao,wala sitakumbuka tena dhambi zao.”
13. Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.