Nahumu 1:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Watateketezwa kama kichaka cha miiba,kama vile nyasi zilizokauka.

11. Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungualiyefanya njama za ulaghai.

12. Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,wao wataangushwa na kuangamizwa.Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,sitawateseni tena zaidi.

13. Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu,na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.”

14. Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi:“Hutapata wazawa kulidumisha jina lako.Sanamu zako za kuchonga na za kusubu,nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako.Mimi nitakuchimbia kaburi lako,maana wewe hufai kitu chochote.”

Nahumu 1