Mwanzo 48:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Lakini baba yake akakataa, akisema, “Najua, mwanangu, najua. Wana wa Manase pia watakuwa taifa kubwa na mashuhuri. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, na wazawa wake watakuwa mataifa mengi.”

20. Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema,“Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia,watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’”Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase.

21. Kisha Israeli akamwambia Yosefu, “Kama uonavyo, mimi niko karibu kufa. Hata hivyo, Mungu atakuwa pamoja nanyi, na kuwarudisheni katika nchi ya babu zenu.

22. Zaidi ya hayo, nimekupa wewe, wala si ndugu zako, eneo moja milimani, nililowanyanganya Waamori kwa upanga na upinde wangu.”

Mwanzo 48