4. Wakati huo wa miaka arubaini nguo zenu hazikuchakaa, wala miguu yenu haikuvimba.
5. Kumbukeni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawarudi kama vile baba amrudivyo mwanawe.
6. Hivyo, shikeni amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpate kuzifuata njia zake na kumcha yeye.
7. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawaleteni kwenye nchi nzuri, nchi yenye vijito na chemchemi, na maji yabubujikayo kutoka bondeni na milimani;
8. nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu, mitini, mikomamanga, mizeituni na asali.