5. Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli,wakati viongozi wao walipokutana,na makabila yote yalipokusanyika.
6. Mose alisema juu ya kabila la Reubeni:“Reubeni aishi wala asife,na watu wake wasiwe wachache.”
7. Juu ya kabila la Yuda alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu usikilize kilio cha kabila la Yuda;umrudishe tena kwa watu wale wengine.Upigane kwa mikono yako kwa ajili yake,ulisaidie kabila la Yuda dhidi ya adui zake.”
8. Juu ya kabila la Lawi, alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu ulipatie Lawi kauli yako ya Urimu,kauli yako ya thumimu kwa hao waaminifu wako,ambao uliwajaribu huko Masa.
9. Ulishindana nao kwenye maji ya Meriba.Walawi walioamua kuwaacha wazee wao,wakawasahau jamaa zao,wasiwatambue hata watoto waomaana walizingatia amri zako,na kushika agano lako.
10. Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.Walawi na wafukize ubani mbele yako,sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.