36. Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake,na kuwahurumia watumishi wake,wakati atakapoona nguvu zao zimeishia,wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.
37. Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake,‘Iko wapi ile miungu yenu,mwamba mlioukimbilia usalama?’
38. Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenuna kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji?Basi na iinuke, iwasaidieni;acheni hiyo iwe kinga yenu sasa!
39. Oneni kuwa mimi ndimi Munguna wala hakuna mwingine ila mimi.Mimi huua na kuweka hai;hujeruhi na kuponya,na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu.