Kumbukumbu La Sheria 28:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

2. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo;

3. “Miji yenu itabarikiwa na mashamba yenu.

4. “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi.

5. “Vikapu vyenu vya nafaka vitabarikiwa na vyombo vyenu vya kukandia.

Kumbukumbu La Sheria 28