Kumbukumbu La Sheria 28:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

2. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo;

3. “Miji yenu itabarikiwa na mashamba yenu.

4. “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi.

Kumbukumbu La Sheria 28