Kumbukumbu La Sheria 1:44-46 Biblia Habari Njema (BHN)

44. Hapo, Waamori waliokuwa wanaishi katika eneo hilo la milimani wakateremka kuwashambulia na kama wafanyavyo nyuki wakawapiga huko Seiri mpaka Horma.

45. Ndipo mliporudi, mkamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini Mwenyezi-Mungu hakuwasikiliza wala hakuwajali.

46. Basi, mkabaki huko Kadeshi kwa muda mrefu ambao mlikaa huko.

Kumbukumbu La Sheria 1