Isaya 65:20-25 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga,wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao.Akifa mtu wa miaka 100 amekufa akiwa kijana;na akifa kabla ya miaka 100 ni balaa.

21. Watu watajenga nyumba na kuishi humo;watalima mizabibu na kula matunda yake.

22. Hawatajenga nyumba zikaliwe na watu wengine,wala kulima chakula kiliwe na watu wengine.Maana watu wangu niliowachaguawataishi maisha marefu kama miti;wateule wangu watafurahia matunda ya jasho lao.

23. Kazi zao hazitakuwa bure,wala hawatazaa watoto wa kupata maafa;maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu,wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.

24. Hata kabla hawajaniita, mimi nitawaitikia;kabla hawajamaliza kusema, nitakuwa nimewajibu.

25. Mbwamwitu na kondoo watakula pamoja,simba watakula nyasi kama ng'ombe,nao nyoka chakula chao kitakuwa vumbi.Katika mlima wangu wote mtakatifu,hakuna atakayeumiza au kuharibu kitu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Isaya 65