3. Imarisheni mikono yenu dhaifu,kazeni magoti yenu manyonge.
4. Waambieni waliokufa moyo:“Jipeni moyo, msiogope!Tazameni Mungu wenu atakuja kulipiza kisasi,atakuja kuwaadhibu maadui zenu;atakuja yeye mwenyewe kuwaokoeni.”
5. Hapo vipofu wataona tena,na viziwi watasikia tena.
6. Walemavu watarukaruka kama paa,na bubu wataimba kwa furaha.Maji yatabubujika nyikanina vijito vya maji jangwani.