8. Aliwaadhibu watu wake kwa kuwapeleka uhamishoni.Wakati wa upepo mkali wa mashariki,aliwaondoa kwa kipigo kikali.
9. Hivi ndivyo uovu wa wazawa wa Yakobo utakavyoondolewa,hivi ndivyo dhambi yake itakavyofutwa kabisa:Ataziharibu madhabahu za miungu;mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa;Ashera, wala madhabahu za kufukizia ubani hazitabaki.
10. Mji ule wa ngome sasa umekuwa mtupu,umeachwa na kuhamwa kama jangwa,humo ndama wanalisha na kupumzika.
11. Matawi ya miti yamekauka na kuvunjika;kina mama huyaokota wakawashia moto.Watu hawa hawajaelewa kitu,kwa hiyo Mungu, Muumba wao, hatawahurumia,yeye aliyewafanya, hatawafadhili.
12. Siku hiyo, kutoka mto Eufrate hadi mpakani mwa Misri, Mwenyezi-Mungu ataipura nafaka yake, nanyi Waisraeli mtakusanywa mmojammoja.