Isaya 18:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Maana, kabla ya mavuno,wakati wa kuchanua umekwisha,maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu,Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea,na kuyakwanyua matawi yanayotanda.

6. Yote yataachiwa ndege milimani,na wanyama wengine wa porini.Ndege walao nyama watakaa humowakati wa majira ya kiangazi,na wanyama wa porini watafanya makao humowakati wa majira ya baridi.”

7. Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

Isaya 18