4. utaimba utenzi huu wa kumdhihaki mfalme wa Babuloni:“Jinsi gani mdhalimu alivyokomeshwa!Ujeuri wake umekomeshwa!
5. Mwenyezi-Mungu amelivunja gongo la waovu,ameivunja fimbo ya kifalme ya watawala,
6. ambao walipiga nayo watu kwa hasira bila kukoma,na kuwatawala kwa udhalimu bila huruma.
7. Sasa dunia yote ina utulivu na amani,kila mtu anaimba kwa furaha.
8. Misonobari inafurahia kuanguka kwako,nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema:‘Kwa vile sasa umeangushwa,hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’