Maana mfalme wa Ashuru alisema:“Kwa nguvu zangu mwenyewe nimetenda hayo,na kwa hekima yangu, maana mimi ni mwerevu!Nimeondoa mipaka kati ya mataifa,nikazipora hazina zao;kama fahali nimewaporomosha walioketia viti vya enzi.