Hosea 7:4-13 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Wote ni wazinzi;wao ni kama tanuri iliyowashwa motoambao mwokaji hauchochei tangu akande ungampaka mkate utakapoumuka.

5. Kwenye sikukuu ya mfalme,waliwalewesha sana maofisa wake;naye mfalme akashirikiana na wahuni.

6. Kama tanuri iwakavyo,mioyo yao huwaka kwa hila;usiku kucha hasira yao hufuka moshi,ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.

7. Wote wamewaka hasira kama tanuri,na wanawaangamiza watawala wao.Wafalme wao wote wameanguka,wala hakuna anayeniomba msaada.

8. “Efraimu amechanganyika na watu wa mataifa.Anaonekana kama mkate ambao haukugeuzwa.

9. Wageni wamezinyonya nguvu zake,wala yeye mwenyewe hajui;mvi zimetapakaa kichwani mwake,lakini mwenyewe hana habari.

10. Kiburi cha Waisraeli chashuhudia dhidi yao,hawanirudii mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao;wala hawanitafuti kwa matukio hayo yote.

11. Efraimu ni kama njiwa, mjinga asiye na akili;mara yuko Misri, mara Ashuru kuomba.

12. Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase,nitawaangusha chini kama ndege wa angani;nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.

13. Ole wao kwa kuwa wameniacha!Maangamizi na yawapate, maana wameniasi.Nilitaka kuwakomboa,lakini wanazua uongo dhidi yangu.

Hosea 7