Hosea 7:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu,ninapotaka kuwaponya Waisraeli,uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa,matendo mabaya ya Samaria hujitokeza.Wao huongozwa na udanganyifu,kwenye nyumba wezi huvunjanje barabarani wanyang'anyi huvamia.

2. Hawafikiri hata kidogo kwamba miminayakumbuka maovu yao yote.Sasa maovu yao yamewabana.Yote waliyotenda yako mbele yangu.

3. “Wanamfurahisha mfalme kwa maovu yaowanawafurahisha wakuu kwa uhaini wao.

4. Wote ni wazinzi;wao ni kama tanuri iliyowashwa motoambao mwokaji hauchochei tangu akande ungampaka mkate utakapoumuka.

5. Kwenye sikukuu ya mfalme,waliwalewesha sana maofisa wake;naye mfalme akashirikiana na wahuni.

6. Kama tanuri iwakavyo,mioyo yao huwaka kwa hila;usiku kucha hasira yao hufuka moshi,ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.

7. Wote wamewaka hasira kama tanuri,na wanawaangamiza watawala wao.Wafalme wao wote wameanguka,wala hakuna anayeniomba msaada.

8. “Efraimu amechanganyika na watu wa mataifa.Anaonekana kama mkate ambao haukugeuzwa.

Hosea 7