Hesabu 32:31-40 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Watu wa Gadi na wa Reubeni wakajibu, “Bwana, sisi tutafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyotuambia sisi watumishi wako.

32. Chini ya uongozi wake Mwenyezi-Mungu, tutavuka na silaha zetu mpaka nchini Kanaani, lakini nchi tuliyopewa hapa mashariki ya Yordani itakuwa mali yetu.”

33. Basi, Mose akawapa watu wa makabila ya Gadi na Reubeni na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu, nchi yote ya mfalme Sihoni wa Waamori na nchi ya mfalme Ogu wa Bashani pamoja na miji na maeneo yaliyokuwa kandokando ya miji hiyo.

34. Kabila la Reubeni likaijenga miji ya Diboni, Atarothi, Aroeri,

35. Atroth-shofani, Yazeri, Yogbeha,

36. Beth-nimra na Beth-harani, miji yenye ngome na mazizi ya kondoo.

37. Kabila la Gadi lilijenga miji ya Heshboni, Eleale, Kiriathaimu,

38. Nebo na Baal-meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa), na Sibma. Miji waliyoijenga waliipa majina mengine.

39. Wazawa wa Makiri, mwana wa Manase, waliishambulia nchi ya Gileadi, wakaiteka na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanakaa humo.

40. Kwa hiyo, Mose akawapa watu wa ukoo wa Makiri mwana wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa humo.

Hesabu 32