Hesabu 24:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungumtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu,mtu anayesujudu na kuona wazi.

5. Hema zako zapendeza namna gani enyi watu wa Yakobo;naam, kambi zenu enyi watu wa Israeli!

6. Ni kama mabonde yanayotiririka maji,kama bustani kandokando ya mto,kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu,kama mierezi kandokando ya maji.

7. Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji,mbegu yao itapata maji mengi,mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi,na ufalme wake utatukuka sana.

8. Mungu aliwachukua kutoka Misri,naye huwapigania kwa nguvu kama nyati.Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao,atavunjavunja mifupa yao,atawachoma kwa mishale yake.

9. Ataotea na kulala chini kama simba,nani atathubutu kumwamsha?Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli,alaaniwe yeyote atakayewalaani.

10. Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki!

Hesabu 24