Amosi 9:9-15 Biblia Habari Njema (BHN)

9. “Tazama, nitatoa amri,na kuwapepeta Waisraeli kati ya mataifakama mtu achekechavyo nafakaniwakamate wote wasiofaa.

10. Wenye dhambi miongoni mwa watu wangu,watafia vitani kwa upanga;hao ndio wasemao:‘Maafa hayatatukumba wala kutupata!’

11. “Siku yaja nitakapoisimika nyumba ya Daudi iliyoanguka;nitazitengeneza kuta zake,na kusimika upya magofu yake.Nitaijenga upya kama ilivyokuwa hapo zamani.

12. Nao Waisraeli watamiliki mabaki ya Edomuna mataifa yote yaliyokuwa yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema,na nitafanya hivyo.

13. “Wakati waja kwa hakika,ambapo mara baada ya kulimamavuno yatakuwa tayari kuvunwa;mara baada ya kupanda mizabibuutafuata wakati wa kuvuna zabibu.Milima itabubujika divai mpya,navyo vilima vitatiririka divai.

14. Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli.Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo;watapanda mizabibu na kunywa divai yake;watalima mashamba na kula mazao yake.

15. Nitawasimika katika nchi yao,wala hawatang'olewa tenakutoka katika nchi niliyowapa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Amosi 9