Amosi 8:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Niliona kikapu kilichojaa matunda ya kiangazi.

2. Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli.Sitavumilia tena maovu yao.

3. Siku hiyo, nyimbo za ikulu zitakuwa maombolezo.Kutakuwa na maiti nyingi,nazo zitatupwa nje kimyakimya.”

4. Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyongena kuwaletea maangamizi fukara wa nchi.

5. Mnajisemea mioyoni mwenu:“Sikukuu ya mwezi mwandamo itakwisha liniili tuanze tena kuuza nafaka yetu?Siku ya Sabato itakwisha liniili tupate kuuza ngano yetu?Tutatumia vipimo hafifu vya wastani na uzito,tutadanganya watu kwa mizani isizo sawa,

6. hata kuuza ngano hafifu kwa bei kubwa.Tutaweza kununua watu fukara kwa fedha,na wahitaji kwa jozi ya kandambili.”

7. Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa:“Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.

Amosi 8