Amosi 5:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikilizeni maombolezo yangu juu yenu,enyi Waisraeli:

2. Umeanguka na hutainuka tenaewe binti Israeli!Umeachwa pweke nchini mwako,hamna hata mtu wa kukuinua.

3. Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupiganalakini watarejea 100 tu;wataondoka watu 100 wa kijiji kimojalakini watanusurika watu kumi tu.”

4. Mwenyezi-Mungu awaambia hivi Waisraeli:“Nitafuteni mimi nanyi mtaishi!

5. Lakini msinitafute huko Betheliwala msiende Gilgaliwala msivuke kwenda Beer-sheba.Maana wakazi wa Gilgali,hakika watachukuliwa uhamishoni,na Betheli utaangamizwa!”

6. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi!La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto;moto utawateketeza wakazi wa Bethelina hakuna mtu atakayeweza kuuzima.

7. Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu,na kuuona uadilifu kuwa kama takataka!

8. Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni,ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana,na mchana kuwa usiku;yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya baharina kuyamwaga juu ya nchi kavu,Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.

Amosi 5