Amosi 5:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikilizeni maombolezo yangu juu yenu,enyi Waisraeli:

2. Umeanguka na hutainuka tenaewe binti Israeli!Umeachwa pweke nchini mwako,hamna hata mtu wa kukuinua.

3. Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupiganalakini watarejea 100 tu;wataondoka watu 100 wa kijiji kimojalakini watanusurika watu kumi tu.”

4. Mwenyezi-Mungu awaambia hivi Waisraeli:“Nitafuteni mimi nanyi mtaishi!

5. Lakini msinitafute huko Betheliwala msiende Gilgaliwala msivuke kwenda Beer-sheba.Maana wakazi wa Gilgali,hakika watachukuliwa uhamishoni,na Betheli utaangamizwa!”

6. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi!La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto;moto utawateketeza wakazi wa Bethelina hakuna mtu atakayeweza kuuzima.

Amosi 5