Amosi 1:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi,waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.

14. Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Raba,na kuziteketeza kabisa ngome zake.Siku hiyo ya vita patakuwa na makelele mengi,nayo mapambano yatakuwa makali kama tufani.

15. Mfalme wao na maofisa wake,wote watakwenda kukaa uhamishoni.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Amosi 1