1 Mambo Ya Nyakati 6:70-75 Biblia Habari Njema (BHN)

70. Katika nusu ya kabila la Manase walipewa miji ya Aneri pamoja na malisho yake, na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ndiyo miji iliyopewa jamaa za ukoo wa Kohathi.

71. Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.

72. Katika kabila la Isakari walipewa: Kedeshi pamoja na malisho yake, Deberathi pamoja na malisho yake,

73. Ramothi pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake.

74. Katika kabila la Asheri walipewa: Mashali pamoja na malisho yake, Abdoni pamoja na malisho yake,

75. Hukoki pamoja na malisho yake, na Rehobu na malisho yake.

1 Mambo Ya Nyakati 6