1 Mambo Ya Nyakati 3:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.

6. Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti,

7. Noga, Nefegi, Yafia,

8. Elishama, Eliada na Elifeleti.

9. Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.

10. Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati,

11. aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi,

12. aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu,

1 Mambo Ya Nyakati 3