6. Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
7. Kura ya 1 ilimwangukia Yoaribu; ya 2 Yedaya;
8. ya 3 Harimu; ya 4 Seorimu;
9. ya 5 Malkia; ya 6 Miyamini;
10. ya 7 Hakosi; ya 8 Abiya;
11. ya 9 Yeshua; ya 10 Shekania;
12. ya 11 Eliashibu; ya 12 Yakimu;
13. ya 13 Hupa; ya 14 Yeshebeabu;
14. ya 15 Bilga; ya 16 Imeri;
15. ya 17 Heziri; ya 18 Hapisesi;
16. ya 19 Pethahia; ya 20 Yehezkeli;
17. ya 21 Yakini; ya 22 Gamuli;
18. ya 23 Delaya; na ya 24 Maazia.
19. Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
20. Hawa ndio wazawa wengine wa Lawi: Mmoja wa wazawa wa Amramu alikuwa Shubaeli; wa Shubaeli alikuwa Yedeya.