5. Waligawanywa kwa kura kwani kulikuwa na wakuu wa mahali patakatifu na viongozi wa kidini miongoni mwa koo zote mbili, yaani ukoo wa Eleazari na ukoo wa Ithamari.
6. Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
7. Kura ya 1 ilimwangukia Yoaribu; ya 2 Yedaya;
8. ya 3 Harimu; ya 4 Seorimu;
9. ya 5 Malkia; ya 6 Miyamini;
10. ya 7 Hakosi; ya 8 Abiya;
11. ya 9 Yeshua; ya 10 Shekania;
12. ya 11 Eliashibu; ya 12 Yakimu;
13. ya 13 Hupa; ya 14 Yeshebeabu;
14. ya 15 Bilga; ya 16 Imeri;
15. ya 17 Heziri; ya 18 Hapisesi;
16. ya 19 Pethahia; ya 20 Yehezkeli;
17. ya 21 Yakini; ya 22 Gamuli;
18. ya 23 Delaya; na ya 24 Maazia.
19. Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
20. Hawa ndio wazawa wengine wa Lawi: Mmoja wa wazawa wa Amramu alikuwa Shubaeli; wa Shubaeli alikuwa Yedeya.
21. Mmoja wa wazawa wa Rehabia alikuwa Ishio kiongozi wa ukoo.
22. Mmoja wa wazawa wa Ishio alikuwa Shelomithi na wa wazawa wa Shelomithi alikuwa Yahathi.
23. Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria wa kwanza, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yakameamu wa nne.
24. Mmoja wa wana wa Uzieli alikuwa Mika. Mmoja wa wazawa wa Mika alikuwa Shamire.