1 Mambo Ya Nyakati 2:51-55 Biblia Habari Njema (BHN)

51. wa pili Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu, na wa tatu Herefu, mwanzilishi wa mji wa Bethi-gaderi.

52. Shobali, mwanzilishi wa mji wa Kiriath-yearimu, alikuwa pia babu yao watu wa Haroe, na nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,

53. pamoja na koo zifuatazo zilizoishi Kiriath-yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. (Wasorathi na Waeshtaoli walitokana na watu hao).

54. Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu alikuwa babu ya Wanetofathi, Waatroth-beth-yoabu na nusu ya Wamenahathi yaani Wasori.

55. Jamaa zifuatazo za waandishi ziliishi katika mji wa Yabesi: Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Wao ndio Wakeni waliotoka katika uzao wa Hamathi, aliyekuwa babu yao waliokuwa wa ukoo wa Warekabu.

1 Mambo Ya Nyakati 2