1. BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,Nimwogope nani?BWANA ni ngome ya uzima wangu,Nimhofu nani?
2. Watenda mabaya waliponikaribia,Wanile nyama yangu,Watesi wangu na adui zangu,Walijikwaa wakaanguka.
3. Jeshi lijapojipanga kupigana nami,Moyo wangu hautaogopa.Vita vijaponitokea,Hata hapo nitatumaini.
4. Neno Moja nimelitaka kwa BWANA,Nalo ndilo nitakalolitafuta,Nikae nyumbani mwa BWANASiku zote za maisha yangu,Niutazame uzuri wa BWANA,Na kutafakari hekaluni mwake.