Yer. 48:29-34 Swahili Union Version (SUV)

29. Tumesikia habari za kiburi cha Moabu;Ya kuwa ana kiburi kingi;Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake,Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake.

30. Najua ghadhabu yake, asema BWANA, ya kuwa si kitu; majisifu yake hayakutenda neno lo lote.

31. Kwa sababu hiyo nitampigia yowe Moabu, naam, nitapiga kelele kwa ajili ya Moabu yote; nitawaombolezea watu wa Kir-heresi.

32. Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hata bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.

33. Furaha na shangwe zimeondoshwa, katika shamba lizaalo sana, na katika nchi ya Moabu; nami nimeikomesha divai katika mashinikizo; hapana mtu atakayekanyaga zabibu kwa shangwe; shangwe ile itakuwa si shangwe.

34. Toka kilio cha Heshboni mpaka Eleale, naam, mpaka Yahasa, wametoa sauti zao, toka Soari mpaka Horonaimu, hata Eglath-shelishia; maana maji ya Nimrimu nayo yatakuwa ukiwa.

Yer. 48