Yer. 48:13-30 Swahili Union Version (SUV)

13. Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, matumaini yao.

14. Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.

15. Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.

16. Msiba wa Moabu umefika karibu,Na mateso yake yanafanya haraka.

17. Ninyi nyote mnaomzunguka, mlilieni,Nanyi nyote mlijuao jina lake, semeni,Jinsi ilivyovunjika fimbo ya enzi,Fimbo ile iliyokuwa nzuri!

18. Ee binti ukaaye Diboni,Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu;Maana atekaye Moabu amepanda juu yako,Ameziharibu ngome zako.

19. Wewe ukaaye Aroeri,Simama kando ya njia upeleleze;Mwulize mwanamume akimbiaye na mwanamke atorokaye,Sema, Imetendeka nini?

20. Moabu ameaibishwa, kwa maana amevunjika;Pigeni yowe na kulia;Tangazeni habari hii katika Arnoni,Ya kuwa Moabu ameharibika.

21. Na hukumu imeifikilia nchi tambarare; juu ya Holoni, na juu ya Yasa, na juu ya Mefaathi;

22. na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;

23. na juu ya Kiriathaimu, na juu ya Beth-gamuli, na juu ya Beth-meoni;

24. na juu ya Keriothi, na juu ya Bozra, na juu ya miji yote ya nchi ya Moabu, iliyo mbali na iliyo karibu.

25. Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema BWANA. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya BWANA

26. na Moabu atagaa-gaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?

27. Alionekana kati ya wevi? Maana kila umtajapo watikisa kichwa chako.

28. Enyi mkaao Moabu, iacheni miji,Enendeni kukaa majabalini;Mkawe kama njiwa afanyaye kioto chakeKatika ubavu wa mdomo wa shimo.

29. Tumesikia habari za kiburi cha Moabu;Ya kuwa ana kiburi kingi;Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake,Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake.

30. Najua ghadhabu yake, asema BWANA, ya kuwa si kitu; majisifu yake hayakutenda neno lo lote.

Yer. 48