7. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,Wala mito haiwezi kuuzamisha;Kama mtu angetoa badala ya upendoMali yote ya nyumbani mwake,Angedharauliwa kabisa.
8. Kwetu sisi tuna umbu mdogo,Wala hana maziwa;Tumfanyieje umbu letu,Siku atakapoposwa?
9. Kama akiwa tu ukuta,Tumjengee buruji za fedha;Na kama akiwa ni mlango,Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.
10. Mimi nalikuwa ukuta,Na maziwa yangu kama minara;Ndipo nikawa machoni pakeKama mtu aliyeipata amani.
11. Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomiAkawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu;Kila mtu atoe vipande elfu vya fedha kwa matunda yake.
12. Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, li mbele yangu.Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako,Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.
13. Wewe ukaaye bustanini,Hao rafiki huisikiliza sauti yako;Unisikizishe mimi.
14. Ukimbie, mpendwa wangu,Nawe uwe kama paa, au ayala,Juu ya milima ya manukato.