Omb. 3:51-66 Swahili Union Version (SUV)

51. Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu,Kwa sababu ya binti zote za mji wangu.

52. Walio adui zangu bila sababuWameniwinda sana kama ndege;

53. Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani,Na kutupa jiwe juu yangu.

54. Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu,Nikasema, Nimekatiliwa mbali.

55. Naliliitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimoLiendalo chini kabisa.

56. Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lakoIli usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

57. Ulinikaribia siku ile nilipokulilia;Ukasema, Usiogope.

58. Ee BWANA umenitetea mateto ya nafsi yangu;Umeukomboa uhai wangu.

59. Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA;Unihukumie neno langu.

60. Umekiona kisasi chao chote,Na mashauri yao yote juu yangu.

61. Ee BWANA, umeyasikia matukano yao,Na mashauri yao yote juu yangu;

62. Midomo yao walioinuka juu yanguNa maazimio yao juu yangu mchana kutwa.

63. Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao;Wimbo wao ndio mimi.

64. Utawalipa malipo, Ee BWANA,Sawasawa na kazi ya mikono yao.

65. Utawapa ushupavu wa moyo;Laana yako juu yao.

66. Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamizaWasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.

Omb. 3