Mit. 25:16-24 Swahili Union Version (SUV)

16. Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;Usije ukashiba na kuitapika.

17. Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi;Asije akakukinai na kukuchukia.

18. Mtu amshuhudiaye jirani yake uongoNi nyundo, na upanga, na mshale mkali.

19. Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabuNi kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.

20. Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito,Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi;Ni kama siki juu ya magadi.

21. Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula;Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;

22. Maana utatia makaa ya moto kichwani pake;Na BWANA atakupa thawabu.

23. Upepo wa kusi huleta mvua;Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.

24. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

Mit. 25