Isa. 52:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;Jivike mavazi yako mazuri,Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yakoAsiyetahiriwa, wala aliye najisi.

2. Jikung’ute mavumbi; uondoke,Uketi, Ee Yerusalemu;Jifungulie vifungo vya shingo yako,Ee binti Sayuni uliyefungwa.

3. Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.

4. Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu.

5. Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.

6. Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.

Isa. 52