11. Kwani ameilegeza kamba yake, na kunitesa,Wala hawajizuii tena mbele yangu.
12. Kwa mkono wangu wa kuume huinuka kundi;Huisukuma miguu yangu kando,Na kunipandishia njia zao za uharibifu.
13. Waiharibu njia yangu,Wauzidisha msiba wangu,Watu wasio na msaidizi.
14. Wanijilia kama wapitao katika ufa mpana;Katikati ya magofu wanishambulia.
15. Vitisho vimenigeukia;Huifukuza heshima yangu kama upepo;Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
16. Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;Siku za mateso zimenishika.
17. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.