13. Tena walikuwa juu ya wachukuzi wa mizigo, wakawahimiza wote waliotenda kazi ya huduma yo yote; na miongoni mwa Walawi kulikuwa na waandishi, na wasimamizi, na mabawabu.
14. Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha torati ya BWANA iliyotolewa kwa mkono wa Musa.
15. Akajibu Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, Kitabu cha torati nimekiona nyumbani mwa BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu.
16. Shafani akampelekea mfalme hicho kitabu, tena akampasha mfalme habari, akisema, Yote waliyokabidhiwa watumishi wako, wayafanya.
17. Nao wameimimina fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA, nayo wameitia mikononi mwa wasimamizi, na mikononi mwa watenda kazi.
18. Shafani mwandishi akamweleza mfalme, akisema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akasoma ndani yake mbele ya mfalme.
19. Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya torati, aliyararua mavazi yake.
20. Mfalme akawaamuru Hilkia, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Abdoni, mwana wa Mika, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme, kusema,
21. Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
22. Basi Hilkia, na hao waliotumwa na mfalme, wakamwendea Hulda nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tohathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi; (naye alikuwa akikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili); wakasema naye kama hayo.
23. Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu huyo aliyewatuma kwangu,
24. BWANA asema hivi, Angalia, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, na juu ya wakaao, laana zote zilizoandikwa katika kitabu hicho walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda;
25. kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.
26. Lakini mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumwuliza BWANA, mtamwambia hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kwa habari ya maneno uliyoyasikia,