10. Wakaitia mikononi mwa watenda kazi walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao mafundi waliotenda kazi nyumbani mwa BWANA wakaitoa kwa kuitengeneza na kuifanya upya nyumba;
11. wakawapa maseremala na waashi, ili wanunue mawe ya kuchonga, na miti ya kuungia, na kuifanyiza boriti kwa nyumba zile walizoziharibu wafalme wa Yuda.
12. Nao watu wakatenda kazi kwa uaminifu; na wasimamizi wao walikuwa Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, wa wana wa Wakohathi, ili kuihimiza kazi; na wengine katika Walawi, wote waliokuwa wastadi wa kupiga vinanda.
13. Tena walikuwa juu ya wachukuzi wa mizigo, wakawahimiza wote waliotenda kazi ya huduma yo yote; na miongoni mwa Walawi kulikuwa na waandishi, na wasimamizi, na mabawabu.
14. Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha torati ya BWANA iliyotolewa kwa mkono wa Musa.
15. Akajibu Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, Kitabu cha torati nimekiona nyumbani mwa BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu.
16. Shafani akampelekea mfalme hicho kitabu, tena akampasha mfalme habari, akisema, Yote waliyokabidhiwa watumishi wako, wayafanya.
17. Nao wameimimina fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA, nayo wameitia mikononi mwa wasimamizi, na mikononi mwa watenda kazi.
18. Shafani mwandishi akamweleza mfalme, akisema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akasoma ndani yake mbele ya mfalme.
19. Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya torati, aliyararua mavazi yake.
20. Mfalme akawaamuru Hilkia, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Abdoni, mwana wa Mika, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme, kusema,
21. Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
22. Basi Hilkia, na hao waliotumwa na mfalme, wakamwendea Hulda nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tohathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi; (naye alikuwa akikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili); wakasema naye kama hayo.
23. Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu huyo aliyewatuma kwangu,