9. Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai.
10. Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye BWANA akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.
11. Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
12. Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.
13. Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni.
14. Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; uwageukie mbali, ukawajie huko kuielekea miforsadi.