1 Fal. 16:31-33 Swahili Union Version (SUV)

31. Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.

32. Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.

33. Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.

1 Fal. 16