1. Niliona maono mengine tena. Safari hii, niliona magari manne ya farasi yakitoka katikati ya milima miwili ya shaba nyeusi.
2. Gari la kwanza lilikokotwa na farasi wekundu, la pili lilikokotwa na farasi weusi,
3. la tatu lilikokotwa na farasi weupe, na la nne lilikokotwa na farasi wa kijivujivu.