Zaburi 42:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Namwambia Mungu, mwamba wangu:“Kwa nini umenisahau?Yanini niende huko na huko nikiombolezakwa kudhulumiwa na adui yangu?”

10. Nimepondwa kwa matukano yao,wanaponiuliza kila siku:“Yuko wapi, Mungu wako!”

11. Mbona nasononeka hivyo moyoni?Kwa nini nahangaika hivyo?Nitamtumainia Mungu,maana nitamsifu tena Mungu,aliye msaada wangu na Mungu wangu.

Zaburi 42