Zaburi 23:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya.Huniongoza katika njia sawakwa hisani yake.

4. Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo,sitaogopa hatari yoyote,maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami;gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

5. Umeniandalia karamu mbele ya maadui zangu;umenipaka mafuta kichwani pangu;kikombe changu umekijaza mpaka kufurika.

6. Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami,siku zote za maisha yangu;nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.

Zaburi 23