Zaburi 18:5-11 Biblia Habari Njema (BHN)

5. kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.

6. Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu,nilimlilia Mungu wangu anisaidie.Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake;kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

7. Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika;misingi ya milima ikayumbayumba,kwani Mungu alikuwa amekasirika.

8. Moshi ulifuka kutoka puani mwake,moto uunguzao ukatoka kinywani mwake;makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.

9. Aliinamisha anga, akashuka chini;na wingu jeusi chini ya miguu yake.

10. Alipanda kiumbe chenye mabawa akaruka;akapaa kasi juu ya mabawa ya upepo.

11. Alijifunika giza pande zote,mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka.

Zaburi 18