1. Sehemu waliyogawiwa wazawa wa Yosefu kwa kura ilianzia karibu na mto Yordani, mashariki ya chemchemi ya Yeriko, na kupitia jangwani, hadi kwenye sehemu za milima mpaka Betheli.
2. Kutoka Betheli mpaka ulielekea Luzu ukapita Atarothi ambako waliishi Waarki.
3. Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.
4. Wazawa wa Yosefu, yaani kabila la Manase na kabila la Efraimu, walipewa nchi hiyo kuwa milki yao.
5. Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu,