Sehemu waliyogawiwa wazawa wa Yosefu kwa kura ilianzia karibu na mto Yordani, mashariki ya chemchemi ya Yeriko, na kupitia jangwani, hadi kwenye sehemu za milima mpaka Betheli.