1. Yafuatayo ni maeneo ya nchi ambayo walipewa Waisraeli katika nchi ya Kanaani. Kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na wakuu wa koo za makabila ya Waisraeli waliwagawia Waisraeli.
2. Sehemu yao hiyo waligawiwa kwa kura kama vile Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose awape yale makabila tisa na nusu.
3. Mose alikuwa ameyapa yale makabila mawili na nusu sehemu yao mashariki ya Yordani, lakini Walawi hawakuwa wamepewa sehemu yao pamoja nao.