Yoshua 13:13-27 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Hata hivyo, Wageshuri na Wamaaka hawakufukuzwa bali wanaishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo.

14. Mose hakuwapa watu wa kabila la Lawi nchi yoyote. Bali tambiko walizomtolea Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli kwa moto, hizo ndizo zilizokuwa fungu lao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose.

15. Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Reubeni kulingana na jamaa zao,

16. ilikuwa kuanzia Aroeri kando ya bonde la Arnoni na mji uliokuwa katika bonde hilo pamoja na nchi yote ya tambarare ya Medeba.

17. Ilikuwa pia pamoja na Heshboni na miji yake yote iliyo katika sehemu tambarare: Yaani Diboni, Bamoth-baali, Beth-baal-meoni,

18. Yahasa, Kedemothi, Mefaathi,

19. Kiriathaimu, Sibma, Sereth-shahari, huko kilimani bondeni,

20. Beth-peori, miteremko ya mlima Pisga, Beth-yeshimothi

21. na miji yote ya tambarare, nchi yote ya mfalme Sihoni wa Waamori ambaye alitawala huko Heshboni; Mose alikuwa amemshinda huyu Sihoni pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, ambao walitawala nchi kwa niaba ya mfalme Sihoni.

22. Balaamu, mtabiri, mwana wa Beori ambaye Waisraeli walimuua alikuwa mmoja wao.

23. Mpaka wa nchi ya kabila la Reubeni upande wa magharibi ulikuwa mto Yordani. Miji na maeneo yaliyotajwa hapa ndiyo sehemu waliyopewa watu wa koo za kabila la Reubeni.

24. Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Gadi kulingana na koo zao

25. ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni hadi Aroeri iliyo mashariki ya Raba,

26. vilevile kuanzia Heshboni hadi Ramath-mizpe, Betonimu, na kutoka Mahanaimu mpaka wa Debiri,

27. kadhalika miji iliyokuwa katika bonde la Beth-haramu, Beth-nimra, Sukothi na Zafoni na nchi yote iliyokuwa ya mfalme Sihoni wa Heshboni; eneo hilo lilikuwa upande wa mashariki wa Yordani na kupakana na upande wa kusini wa bahari ya Kinerethi.

Yoshua 13